Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Oliver Daniel Semuguruka
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA K.n.y. MHE. ERIC J. SHIGONGO aliuliza: - Je, lini Serikali itafufua kiwanda cha kuchambua Pamba cha Nyakarilo, Buchosa?
Supplementary Question 1
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, naishukuru Serikali kwa majibu mazuri ya Jimbo la Buchosa. Sasa ninalo swali dogo la nyongeza. Je, Serikali ina mpango gani katika kuimarisha Kiwanda cha Maruku cha Chai kilichopo Bukoba Vijijini ambacho kinafanya kazi kwa kusuasua?
Name
Exaud Silaoneka Kigahe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, kwanza, nampongeza sana Mheshimiwa Oliver kwa swali zuri la Sekta ya Kilimo na uongezaji thamani wa mazao ya kilimo ikiwemo chai.
Mheshimiwa Spika, Kiwanda hiki cha Kagera Tea Company ambacho kiko Maruku ni moja ya viwanda katika sekta ya chai. Kama tunavyojua, sekta ya chai ina changamoto kidogo, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali imeshaweka nia thabiti na mikakati ya kuhakikisha kwamba sekta ya chai inakua, kwanza kwa kuviwezesha na kuhakikisha kuwa viwanda vyote vya chai vinafanya kazi vizuri, pamoja na kuhakikisha kwamba tunapata soko kwa sababu changamoto iliyopo kwenye sekta ya chai ni soko linalosuasua.
Mheshimiwa Spika, vilevile, kwenye vile viwanda ambavyo vina changamoto zaidi, tutakaa na wenye viwanda ili tuone namna ya kuwasaidia kwa sababu hivi viwanda ni vya sekta binafsi.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutakuja pale Maruku tukae na huyu mwekezaji ili tuone namna ya kumsaidia pale ambapo ana changamoto katika uchakataji wa chai katika Kampuni hii ya Kagera Tea Company.
Name
Jonas Van Zeeland
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mvomero
Primary Question
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA K.n.y. MHE. ERIC J. SHIGONGO aliuliza: - Je, lini Serikali itafufua kiwanda cha kuchambua Pamba cha Nyakarilo, Buchosa?
Supplementary Question 2
MHE. JONAS V. ZEELAND: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa wakulima wa Kata ya Doma, Msongozi na Mlali ni wakulima wakubwa sana wa zao la nyanya, je, Serikali haioni sasa kuna haja ya kutafuta mwekezaji wa kujenga kiwanda kidogo cha kusindika nyanya ili kuokoa wakulima hawa kwa hasara wanayoipata ya kutafuta soko?
Name
Exaud Silaoneka Kigahe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Nampongeza Mheshimiwa Jonas, ni kweli kama nilivyosema, lengo la Serikali ni kuona mazao yote ya kilimo yanaongezwa thamani ili kuongeza pato kwa wakulima.
Mheshimiwa Spika, moja ya maeneo ambayo tunaangalia ni hili la nyanya na maeneo mengine ya horticulture. Kwa hiyo, tutahakikisha katika eneo hilo nako tutatafuta wawekezaji ili tuweze kuwaleta waweze kuongeza thamani kwenye nyanya ambazo zinapotea (postharvest losses), nakushukuru sana.
Name
Grace Victor Tendega
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA K.n.y. MHE. ERIC J. SHIGONGO aliuliza: - Je, lini Serikali itafufua kiwanda cha kuchambua Pamba cha Nyakarilo, Buchosa?
Supplementary Question 3
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona. Je, ni upi mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kwamba Kiwanda cha Chai cha Kilolo kinafufuliwa? (Makofi)
Name
Exaud Silaoneka Kigahe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Grace kwa swali zuri. Kama nilivyojibu kwenye swali la nyongeza la Mheshimiwa Oliver, Sekta ya Chai ina changamoto, lakini mipango ya Serikali ni kuhakikisha tunakwamua sekta hiyo.
Mheshimiwa Spika, moja ya mikakati ambayo tumeiweka ni kuhakikisha wakulima wa chai Kilolo, kwanza wamewezeshwa. Hatua inayofuata ni kuwatafutia sasa sehemu ya kuongeza thamani na tunapeleka kwenye Kiwanda cha Mufindi Tea Company ambacho kitaongeza thamani kwa maana ya kuchakata chai yao.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mkakati wa Serikali ni kuhakikisha tunawawezesha wakulima hawa kwa kufufua mashamba yale ambayo tayari tumeshaanza kupitia Wizara ya Kilimo. Baadaye tutaenda kupeleka kuzalisha au kuchakata chai kwenye viwanda vya jirani ikiwemo kiwanda cha Mufindi Tea Company, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved