Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 146 2025-02-07

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASIA A. HALAMGA aliuliza:-

Je, lini Wananchi waliolipia upimaji watapewa Hati za umiliki wa Ardhi - Hanang?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, jumla ya mashamba 5,506 yamepimwa katika Kata za Gitting, Masakta, Ishponga, Dirma, Balangdalalu, Gehandu na Mogitu. Aidha, jumla ya viwanja 11,440 vimepimwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang katika kata za Ganana, Endasiwold, Nangwa, Bassotu, Dumbeta, Katesh na Balangdalalu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya upimaji kukamilika, wananchi wameandaliwa nyaraka za umiliki wa ardhi zao ambapo jumla ya Hati za Hakimiliki za Kimila 1,360 zimeandaliwa na kutolewa kwa wananchi wa kata za Gitting (150), Masakta (210) na Ishponga (1,000). Aidha, jumla ya Hatimiliki 1,505 zimeandaliwa na kutolewa katika Kata za Gitting (355), Masakta (205) na Ishponga (950).
Mheshimiwa Spika, zoezi la kuandaa Hatimiliki na Hati za Hakimiliki za Kimila bado linaendelea kutegemeana na ukamilishwaji wa masharti ya umiliki wa ardhi kwa wananchi husika. Aidha, Serikali inaendelea kushughulikia changamoto na malalamiko ya wananchi yanayoendelea kujitokeza wakati wa zoezi la umilikishwaji ardhi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.