Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 147 2025-02-07

Name

Emmanuel Peter Cherehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Primary Question

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka gari Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Kahama ili kuboresha utendaji kazi?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Kahama kwa sasa ina gari moja yenye namba za usajili STL 1022 aina ya Ford Ranger pick - up double cabin ambayo ni chakavu. Aidha, Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji imetenga kiasi cha fedha shilingi 3,259,987,000 katika mwaka wa fedha 2024/2025 kwa ajili ya ununuzi wa magari 18 kwa ajili ya kuimarisha misako na doria nchini. Pindi magari yatakaponunuliwa, yatasambazwa kwenye wilaya zenye uhitaji mkubwa ikiwemo na Wilaya ya Kahama, ahsante.