Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Emmanuel Peter Cherehani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ushetu
Primary Question
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka gari Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Kahama ili kuboresha utendaji kazi?
Supplementary Question 1
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali. Wilaya ya Kahama ina halmashauri tatu; Msalala, Kahama pamoja na Ushetu, lakini imekuwa ndiyo lango la nchi jirani; Congo, Burundi, Rwanda na Uganda.
Mheshimiwa Spika, hawa watu hawana gari zaidi ya miaka minne leo, lakini pia wana pikipiki mbili za kudhibiti uhamiaji kitu ambacho ni hatari sana kwa askari wetu.
Mheshimiwa Spika, nataka nipate commitment ya Serikali kwa sababu nimekuwa nikiahidiwa kila mwaka, na mwaka 2024 gari zilipatikana zikapelekwa pale mkoani. Kwa hiyo, hali ya Kahama siyo nzuri, naomba nipate commitment ya Serikali.
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji wa gari la uhamiaji kwa Ofisi ya Kahama. Ni kweli Wilaya ya Kahama ina Halmashauri tatu kwa maana ya Ushetu, Msalala pamoja na Kahama yenyewe.
Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, tayari tulishapata kibali kwa ajili ya kununua magari 18. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika mgao huu utapata gari kwa ajili ya wilaya yake ya Kahama, ahsante.
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka gari Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Kahama ili kuboresha utendaji kazi?
Supplementary Question 2
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, Serikali ina mkakati gani wa haraka wa kuhakikisha kwamba inapeleka gari kwenye Ofisi ya uhamiaji Tarime pamoja na Ofisi ya Kipolisi ya Nyamwaga na Tarime ambazo hazina magari kabisa ili kurahisisha utendaji?
SPIKA: Ngoja Mheshimiwa swali ni moja. Uliza mojawapo kati ya hayo uliyouliza.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, Serikali ina mkakati gani wa haraka wa kuhakikisha kwamba inapeleka gari kwenye Ofisi ya Uhamiaji Tarime ili kurahisisha utendaji, maana hamna gari kabisa? (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye swali la msingi, tumeagiza magari 18 na tunaanza na wilaya zile za mpakani kwa ajili ya kuimarisha misako na doria. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwenye mgao huu Wilaya ya Tarime pia itakuwa mojawapo kwa sababu ipo pia mpakani, ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved