Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 149 2025-02-07

Name

Amandus Julius Chinguile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nachingwea

Primary Question

MHE. ALLY M. KASSINGE K.n.y. MHE. AMANDUS J. CHINGUILE aliuliza:-

Je, lini Skimu za Umwagiliaji zitajengwa katika Kata za Ruponda, Mramba, Mbondo, Matekwe na Kilimarondo – Nachingwea?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imepanga kuchimba visima na kuweka miundombinu ya umwagiliaji katika maeneo ya Ruponda, Mandawa, Marambo, Mnerongongo na Ntila. Aidha, maeneo ya Matekwe, Mbondo, Kilimarondo na Mitumbati kwa pamoja yatapewa kipaumbele katika mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026, ahsante sana.