Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ally Mohamed Kassinge
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kusini
Primary Question
MHE. ALLY M. KASSINGE K.n.y. MHE. AMANDUS J. CHINGUILE aliuliza:- Je, lini Skimu za Umwagiliaji zitajengwa katika Kata za Ruponda, Mramba, Mbondo, Matekwe na Kilimarondo – Nachingwea?
Supplementary Question 1
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Spika, nina maswali mawili madogo ya nyongeza, lakini pia naishukuru Serikali kwa majibu ambayo yanakwenda kutoa matumaini kwa wananchi wa Nachingwea.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Kwa kuwa maeneo ambayo Mheshimiwa Chinguile ameyaainisha yapo katika bajeti ya 2025/2026, nini commitment ya Serikali kuhakikisha kwamba skimu hizi zinakwenda kujengwa na hazitachukua muda mrefu kama ambavyo ilikuwa huko awali?
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kupitia mpango huu wa kujenga visima katika maeneo ya mabonde ya umwagiliaji, pale Wilayani Kilwa kuna Bonde la Makangaga katika Kata ya Kiranjeranje. Nini commitment ya Serikali kujenga kisima kwa ajili ya umwagiliaji katika Bonde la Makangaga? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Niwathibitishie tu wananchi wa Nachingwea kupitia swali la Mheshimiwa Kassinge kwamba commitment ya Serikali iko palepale, ndiyo maana jambo hili tumeliweka katika bajeti yetu kwamba tumedhamiria kulifanya na tutalifanya kwa kadri pesa zinavyopatikana.
Mheshimiwa Spika, bahati nzuri Wizara ya Fedha imekuwa ikitoa ushirikiano kuleta fedha ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na wananchi wanapata huduma.
Mheshimiwa Spika, kuhusu commitment ya kuchimba kisima katika Bonde la Makangaga katika Jimbo la Kilwa Kusini, nimthibitishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba jambo hilo tutalitekeleza kwa sababu lipo katika mpango wa mwaka wa fedha unaokuja, ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Thea Medard Ntara
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ALLY M. KASSINGE K.n.y. MHE. AMANDUS J. CHINGUILE aliuliza:- Je, lini Skimu za Umwagiliaji zitajengwa katika Kata za Ruponda, Mramba, Mbondo, Matekwe na Kilimarondo – Nachingwea?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, pamoja na juhudi kubwa za Serikali za kupeleka wataalamu katika Maporomoko ya Likingu kule Mdunduwalo, je, Serikali sasa itaanza lini ujenzi wa skimu ili wasomi vijana wa kule waanze kulima zao la mpunga? Ahsante sana.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni kwamba tayari tumeshapeleka wataalamu katika maporomoko ya Likingu ambao wameenda kwa kazi moja tu ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na hatua zilizopo sasa hivi ni kumalizia michoro na baada ya hapo tutangaze hiyo tenda kwa ajili ya kumpata mkandarasi ambaye atapewa hiyo kazi. Kwa hiyo, wananchi wa Jimbo la Peramiho, Songea Vijijini wakae mkao wa utayari kwa ajili ya kazi hiyo, ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Florence George Samizi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Muhambwe
Primary Question
MHE. ALLY M. KASSINGE K.n.y. MHE. AMANDUS J. CHINGUILE aliuliza:- Je, lini Skimu za Umwagiliaji zitajengwa katika Kata za Ruponda, Mramba, Mbondo, Matekwe na Kilimarondo – Nachingwea?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI: Mheshimiwa Spika, Skimu ya Nyendara iliyojengwa katika Jimbo la Muhambwe haikukamilika na hivyo kuacha eneo ambalo ni hatarishi kwa maisha ya binadamu na watoto mara nyingi wanatumbukia. Je, ni lini Serikali italeta fedha ili tukamilishe Skimu ya Nyendara ili watoto wasiathirike zaidi? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nimwondoe shaka Mheshimiwa Mbunge kwamba hatua ya awali ambayo tulikuwa tumeipanga kibajeti katika Skimu ya Lingala, tayari tumeshaifanya, na hatua ya pili ni kufanya expansion ambayo sasa hivi watu wa tume wanaendelea na hatua za mwisho za kufanya ile tunasema feasibility study ili kukamilisha mchoro na kuanzisha ili tuweze kuwasaidia zaidi wakulima katika eneo la jimbo lako, ahsante. (Makofi)
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Primary Question
MHE. ALLY M. KASSINGE K.n.y. MHE. AMANDUS J. CHINGUILE aliuliza:- Je, lini Skimu za Umwagiliaji zitajengwa katika Kata za Ruponda, Mramba, Mbondo, Matekwe na Kilimarondo – Nachingwea?
Supplementary Question 4
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa skimu ya umwagiliaji kwenye Mto Myovizi kwenye Kata ya Mlangali ambayo ni eneo muhimu sana kwa uzalishaji? Ahsante sana.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni kweli anachokisema Mheshimiwa Hasunga, Mbunge wa Jimbo la Vwawa, kwamba Mto Myovizi ni moja ya mto ambao una faida kubwa sana kwa wananchi katika jimbo lake na ni sehemu ya miradi ambayo sisi Wizara ya Kilimo tunaipa kipaumbele na ndiyo maana wataalamu wetu sasa hivi na wenyewe wanafanya feasibility study ili tukamilishe ule mchoro, tutafute fedha ili tujenge mradi ambao utasaidia wananchi wa Kata ya Mlangali kulingana na standard za kisasa.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge wathibitishie wananchi wa eneo hilo kwamba Serikali iko kazini na tutalifikia hili jambo kama ambavyo nimeahidi hapa. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved