Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 150 2025-02-07

Name

Leah Jeremiah Komanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Meatu

Primary Question

MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kutafuta Soko la uhakika la Zao la Alizeti?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na wadau inatekeleza mikakati mbalimbali ya kuhakikisha uwepo wa masoko ya uhakika ya mazao ya kilimo ikiwemo zao la alizeti kwa kuhamasisha kilimo cha kibiashara kinachozingatia mahitaji ya soko; kuhamashisha uanzishwaji wa viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na kuwaunganisha na wakulima; ukamilishaji wa kanuni za kilimo cha mkataba; na kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) kukaa na wadau na kupendekeza bei elekezi ya kununua alizeti kwa kilo pale inapohitajika.