Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Leah Jeremiah Komanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Meatu

Primary Question

MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kutafuta Soko la uhakika la Zao la Alizeti?

Supplementary Question 1

MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa mikakati mizuri ya Serikali. Kwa kuwa, soko la alizeti liko juu sana nchi za nje, pamoja na viwanda vilivyopo nchini, je, Serikali haioni haja ya kumtafuta mwekezaji ambaye atawekeza kufikia soko la nje ili kuleta ushindani katika bei ya alizeti kwa wakulima?

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, mpaka sasa Wilaya ya Meatu hawajapelekewa mbegu za alizeti, je, Serikali haioni haja ya kuwapelekea mbegu za alizeti zenye tija zitakazowatolea mafuta mengi ili wakulima kujiongezea kipato?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, namshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa kuona umuhimu wa wawekezaji nchini. Wizara ya Kilimo tumeshafanya majadiliano na balozi zote za nje ya nchi zinazowakilisha Tanzania kwamba watafute wawekezaji ambao wanaweza kuja kuwekeza hapa nchini katika kuongeza thamani ya zao la alizeti.

Mheshimiwa Spika, vilevile, sisi kama Wizara tumeendelea kutoa wito kwa wawekezaji wa ndani waweze kuwekeza katika zao hilo ili kuongeza thamani na tupate mafuta ya kutosha kwa ajili ya wananchi, kwa sababu bado mahitaji ya ndani ya mafuta ni makubwa sana tofauti yalivyo kule nje. Kwa hiyo, mahitaji ya ndani ya mtakuta ni makubwa sana.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mahitaji ya alizeti katika Jimbo la Meatu, niwaelekeze tu, Agent wetu ASA, Mamlaka ya Uzalishaji wa Mbegu, kwamba wapeleke mbegu katika Halmashauri ya Meatu kwa sababu wanazo mbegu za kutosha za alizeti, hivi ninavyozungumza nina uhakika na hiki ninachokisema, ahsante. (Makofi)