Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 7 | Youth, Disabled, Labor and Employment | Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu | 108 | 2025-02-05 |
Name
Latifa Khamis Juwakali
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. LATIFA KHAMIS JUWAKALI aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kuwatambua Vijana wenye ujuzi ambao hawatambuliki rasmi ili kuwaendeleza?
Name
Paschal Katambi Patrobas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shinyanga Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Latifa Khamis Juwakali, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuwatambua vijana wenye ujuzi ambao hautambuliki kwa kuweka mipango ifuatayo:-
(i) Kuboresha mazingira ya kisera ili kuwawezesha vijana kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuweza kujitegemea kupitia Sera ya Maendeleo ya Vijana (2007) ambayo imefanyiwa marekebisho ikiwa ni Tolea la Mwaka 2024, na Sera ya Taifa ya Ajira ya Mwaka 2008;
(ii) Kurasimisha na kutambua ujuzi wa vijana uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa elimu;
(iii) Kubuni na kutekeleza programu maalum kupitia sekta zinazozalisha ajira kwa wingi kama vile Sekta ya Kilimo kupitia programu ya Jenga Kesho Iliyobora, ujasiriamali, na madini kupitia Programu ya Mining for a Brighter Tomorrow;
(iv) Kuimarisha utoaji wa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wa ngazi za Stashahada na Shahada kupitia maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la Mwaka 2023;
(v) Kujenga miundombinu ya Kimkakati inayochochea uchumi ambayo inakuza ujuzi na inachangia kuzalisha ajira mfano ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere na barabara ya mwendokasi ya SGR;
(vi) Kubuni na kutekeleza programu ya kukuza ujuzi ambayo inalenga kukuza ujuzi kwa nguvu kazi ya Taifa, mfano mafunzo ya kuongeza ujuzi kwa wafanyakazi waliopo kazini na wajasiriamali; na
(vii) Kuweka msisitizo kwenye matumizi ya TEHAMA katika kuzalisha fursa nyingi za ajira kwa vijana.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved