Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 7 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 109 2025-02-05

Name

Silvestry Fransis Koka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibaha Mjini

Primary Question

MHE. SILYVESTRY F. KOKA aliuliza:-

Je, nini hatma ya Shirika la Elimu Kibaha?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Shirika la Elimu Kibaha lilianzishwa mwaka 1963 kwa lengo la kuondoa umaskini, ujinga na maradhi ambapo ilisababisha kuanzisha huduma za elimu, afya na uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, tarehe 15 Disemba, 2023, Serikali ilitangaza kuvunja Shirika la Elimu Kibaha ambapo Hospitali ya Tumbi, Kibaha ilitangazwa kuwa Hospitali ya Mkoa wa Pwani.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kutafuta namna bora ya kuratibu taasisi zilizo chini ya shirika hilo ili kutoathiri lengo kuu la kuanzishwa kwake.