Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Silvestry Fransis Koka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibaha Mjini

Primary Question

MHE. SILYVESTRY F. KOKA aliuliza:- Je, nini hatma ya Shirika la Elimu Kibaha?

Supplementary Question 1

MHE. SILYVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; Shirika hili lina ukubwa wa takribani hekari 3,400 na lengo lake kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri ni kuondoa ujinga, maradhi na umaskini.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa, kama Serikali imeamua kuangalia upya na kulivunja ili kubaini namna bora kuendesha shirika hili, je, ni lini Serikali itakuwa tayari kuleta mkakati huo ili tukawashirikishe wananchi wa Kibaha Mjini?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Manispaa ya Mji wa Kibaha iliomba rasmi angalau hekari 1,500 ili ziendelezwe na kuondoa lile eneo ambalo linaonekana ni pori, likiambatana na Barabara ya Dar es Salaam – Morogoro. Je, ni lini Serikali itatenga eneo hili kwa ajili ya manispaa, ikiwa ni pamoja na mkakati wa kufufua shirika hili ili liweze kuleta tija ya kuondoa umaskini, maradhi na ujinga kama ilivyokusudiwa?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake lenye nia ya kutaka kuwasemea wapiga kura wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nijibu maswali yake mawili kwa pamoja. Ni kweli Serikali ilitangaza kuvunja Shirika hili la Elimu la Kibaha. Hata hivyo, Serikali imefanya mapitio ya maamuzi yake na kuamua kwamba, kutokana na sababu za kihistoria, sababu kubwa kabisa na lengo la kuondoa umaskini, ujinga na maradhi, shirika hili litaendelea kuwepo badala ya kuvunjwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, katika muktadha huo, hoja ya Mheshimiwa Mbunge kuhusu maeneo ya shirika hili ambayo bado hayajaendelezwa na yanatengeneza mwonekano wa pori katika Manispaa ya Kibaha, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itafanya uwekezaji katika Shirika hili la Elimu la Kibaha, ili kuondoa na hadha hiyo ya kuonekana kuna mapori, kutokana na shirika hili kutokuendelezwa na kuwa na eneo kubwa lenye pori.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba shirika litaendelezwa na Kibaha watapata mazingira mazuri kabisa ya mwonekano kwenye shirika hili. (Makofi)