Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 7 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 110 2025-02-05

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI aliuliza:-

Je, ni Shule zipi chakavu katika Jimbo la Vunjo zimewekwa kwenye Mpango wa kufanyiwa ukarabati?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2022/2023, Ofisi ya Rais, TAMISEMI ilifanya tathmini ya mahitaji na hali ya miundombinu ya shule zote za msingi zikiwemo shule za Jimbo la Vunjo. Aidha, kuanzia mwaka 2022/2023 hadi 2023/2024, Serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya ukarabati, ambapo shilingi bilioni 70.39 zimetolewa kwa ajili ya ukarabati wa shule 793 zikijumuisha shilingi bilioni 1.58 zilizokarabati shule za msingi 15 na shule za sekondari tatu zilizopo katika Jimbo la Vunjo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha za ukarabati wa shule chakavu zikiwemo shule za Jimbo la Vunjo kadri ya upatikanaji wa fedha.