Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 7 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 111 2025-02-05

Name

Innocent Edward Kalogeris

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini

Primary Question

MHE. INNOCENT E. KALOGERIS aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga vituo vya afya Kata ya Singisa na Bwakila Juu katika Jimbo la Morogoro Kusini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea na ujenzi wa vituo vya afya katika Kata za Kimkakati kote nchini, ambapo katika Mwaka wa Fedha 2021/2022, Serikali ilipeleka shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kasanga na Mkulazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ambavyo vimeanza kutoa huduma za wagonjwa wa nje (OPD) na majengo kwa ajili ya huduma za upasuaji wa dharura kwa akinamama wajawazito ambapo ujenzi wake upo hatua ya ukamilishaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Singisa ina jumla ya wananchi 14,812, vijiji saba na zahanati moja, hivyo Serikali itafanya tathmini ya Kata hiyo ikiwa inakidhi vigezo vya kata ya kimkakati na mpango wa ujenzi wa kituo cha afya utaandaliwa. Aidha, Kata ya Bwakila juu ina jumla wananchi 6,776, vijiji vitatu na zahanati mbili hivyo haikidhi vigezo vya kuwa na kituo cha afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuboresha zahanati zilizopo katika Kata ya Bwakila Juu ili kusogeza huduma za afya karibu na wananchi. Ahsante.