Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 7 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 112 2025-02-05

Name

Vita Rashid Kawawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Primary Question

MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Kisasa cha Mabasi - Namtumbo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua uhitaji wa kituo cha mabasi katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ili kuboresha huduma za usafiri. Aidha, Halmashauri imefanya tathmini ya ujenzi wa stendi hiyo na kuanza hatua za awali za ujenzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi sasa kazi zilizofanyika ni pamoja na kutenga eneo lenye ukubwa wa ekari 3.18 lililopo eneo la Muungano Namtumbo Mjini na kupata hati miliki ya eneo hilo; kuchonga barabara ya kuingia na kutoka; ujenzi wa baadhi ya miundombinu ya awali ambayo ni jengo dogo la abiria, choo cha abiria na mabanda ya biashara ndogondogo. Kazi hizo zimegharimu jumla ya shilingi milioni 34.7

Mheshimiwa Naibu Spika, halmashauri imekamilisha andiko la mradi huo ikiwa ni pamoja na kukamilisha michoro, ramani na makadirio ya gharama. Mradi huo unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 3.5 na hatua inayofuata ni uwasilishaji wa andiko hilo kwa ajili ya upembuzi na kupata fedha kwa ajili ya ujenzi. Ahsante. (Makofi)