Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 7 Public Service Management Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 113 2025-02-05

Name

Nancy Hassan Nyalusi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE K.n.y. MHE. NANCY H. NYALUSI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa mafunzo kwa Watumishi wa Umma ili kuendana na kasi ya maendeleo na kuongeza ufanisi?

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha watumishi wa umma wanaendelezwa katika taaluma zao ili kuendana na kasi ya maendeleo na kuongeza ufanisi, waajiri wote wanapaswa kuainisha mahitaji ya mafunzo, kuandaa mipango ya mafunzo na kutenga bajeti kila mwaka na kusimamia utekelezaji wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na waajiri kutenga fedha za mafunzo kwa watumishi wa umma, Serikali pia imekuwa ikipokea fursa za mafunzo ya muda mrefu na mfupi kutoka maeneo mbalimbali ya kimkakati kwa kuzingatia vipaumbele vya Kitaifa kutoka kwa wadau mbalimbali wa Maendeleo wakiwemo Korea, China, India, Indonesia, Japan, Singapore, Misri, Malaysia, Thailand na Bangladesh ambapo kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 zaidi ya watumishi 1,278 walinufaika na fursa hizo. Ninakushukuru.