Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 7 Public Service Management Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 114 2025-02-05

Name

Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba kusini

Primary Question

MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwapa posho ya mazingira magumu wafanyakazi hasa walimu wanaopangiwa kazi mikoa ya pembezoni?

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za kuishi walimu hususan walimu wa umma na watumishi wa kada za afya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Pia, ukarabati wa miundombinu ya barabara; kuboresha huduma za jamii kama vile, elimu, afya, maji, nishati ya umeme na mawasiliano ya simu.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, huduma hizi zinawanufaisha watumishi wa umma wote pamoja na wanaofanya kazi katika mikoa ya pembezoni. Hata hivyo, Serikali haijatoa mwongozo mahsusi wa kulipa posho ya mazingira magumu kwa watumishi wa kada ya ualimu na watumishi wengine wa umma wanaopangiwa vituo vya kazi katika mikoa ya pembezoni kutokana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika utekelezaji wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru.