Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 7 Planning and Investment Ofisi ya Rais: Mipango na Uwekezaji 115 2025-02-05

Name

Taska Restituta Mbogo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:-

Je, lini Serikali itawalipa Wastaafu waliokuwa Wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaodai formula haikufuatwa wakati wanalipwa?

Name

Stanslaus Haroon Nyongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Mashariki

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na uhakiki uliofanyika, ilibainika kuwa, wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaoidai Serikali kutokana na dosari ya ukokotozi wa fomula wanadai shilingi bilioni 1.3 ambapo shilingi bilioni 1.17 kwa wastaafu walio hai 146 na shilingi milioni 151.1 kwa wastaafu 21 waliofariki.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya uhakiki, tumewasilisha orodha ya madeni kwa Wizara ya Fedha ili yalipwe pindi pesa zitakapopatikana. Ahsante sana.