Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Taska Restituta Mbogo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, lini Serikali itawalipa Wastaafu waliokuwa Wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaodai formula haikufuatwa wakati wanalipwa?

Supplementary Question 1

MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kuwa wafanyakazi hawa wamekuwa wakiidai Serikali toka mwaka 1977 na wengi wao wamefariki bila kupata mafao yao. Je, Serikali haioni haja ya kuharakisha mchakato wa kuwalipa wafanyakazi hawa? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; waliokuwa wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanadai kwamba Serikali iliwalipa pesa pungufu kinyume na kikokotoo ambacho kilitolewa na Liquidator. Je, Serikali ina mkakati gani wa kukaa nao mezani ili kuangalia madai yao ambayo wanadai na walitakiwa walipwe? (Makofi)

Name

Stanslaus Haroon Nyongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Mashariki

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba niendelee kujibu maswali ya maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Taska Restituta Mbogo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuna wafanyakazi ambao wamedai kwa muda mrefu na wengine wamefariki, lakini msingi wa swali hili ulikuwa ni kufuatilia na kuweza kujua yale mapungufu ya wafanyakazi ambao walikuwa chini ya TTCL kabla na baada ya kubinafsishwa na wengine ambao walipeleka kesi Mahakamani (Kesi Namba 69 ya Mwaka 2005) na wengine ambao walikuwa wafanyakazi wa East Africa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwamba, sisi kupitia Ofisi ya Mtunza Hazina tumeweza kuhakiki madeni hayo na tumegundua kweli, kulikuwa na madeni ambayo yamekosewa kutokana na ukokotoaji, ambayo yalifanya waweze kupata upungufu wa fedha walizokuwa wakilipwa kila mwezi. Tumefuatilia na tumeweza kuhakiki madeni hayo na Ofisi ya TR ilivyoweza kugundua, imekuja na figure hii ya 1.3 billion ambayo sasa tumeipeleka Wizara ya Fedha, ili waweze kuandaa mkakati wa kulipa.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, kuna wafanyakazi wengine ambao kwa kweli, Serikali bado inaendelea kuhakiki (Kwa wale wafanyakazi wengine wa kampuni nyingine ambazo zilikuwa chini ya East Africa na Wafanyakazi wa East Africa kwa ujumla). Tutakapogundua kwamba, kweli kuna watu wanadai fedha hizo, Serikali chini ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, itawalipa wale wote ambao wanadai madeni hayo. Ahsante sana.

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, lini Serikali itawalipa Wastaafu waliokuwa Wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaodai formula haikufuatwa wakati wanalipwa?

Supplementary Question 2

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Nina mwaka wa kumi katika Bunge hili na swali hili limekuwa likiulizwa mara kwa mara. Je, Serikali haioni sasa, ina wajibu wa kufanya haraka iwezekanavyo ili watu hawa waweze kulipwa fedha zao?

Name

Stanslaus Haroon Nyongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Mashariki

Answer

NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuna watu wanadai fedha kwa muda mrefu na wakati mwingine inakuwa ni vigumu kupata vielelezo. Hata hivyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inakwenda kulipa madeni yale yote ambayo yatakuwa yamekwisha kuhakikiwa.