Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 7 Union Affairs Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano 116 2025-02-05

Name

Tunza Issa Malapo

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza:-

Je, Serikali imefanya Tathmini ya kujua ni Miti mingapi inayopandwa inatunzwa na kukua ili kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, imekuwa ikifanya tathmini ya upandaji miti kwa kila mwaka ili kukabiliana na uharibifu wa ardhi, kuenea kwa hali ya jangwa na ukame na kupambana dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha mwaka 2020/2021 – 2023/2024 tathmini imebainisha kuwa, jumla ya miti milioni 866.7 ilipandwa ambapo kati ya miti hiyo, miti milioni 686.24 ilistawi, sawa na 82.3%. Aidha, katika msimu wa mwaka 2024/2025, Serikali inaendelea kufanya tathmini, ili kubaini idadi ya miti iliyopandwa na iliyostawi kwa maeneo yote nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kuhamasisha wananchi na Sekta binafsi kuendelea kupanda miti kwenye maeneo mbalimbali nchini, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kutunza mazingira. Aidha, kupitia Bunge lako Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninaomba kutoa wito kwa jamii nzima ya Watanzania kutumia mvua zinazonyesha kipindi hiki kwa kupanda miti katika maeneo yetu mbalimbali. Nakushukuru.