Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 151 2025-02-07

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itawalipa fidia wananchi waliopisha ujenzi wa Barabara ya Mchepuko kutoka Ifakara, Kikwawila, Mbasa hadi Lipangalala?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa awali wa Barabara ya Mchepuo ya Mji wa Ifakara yenye urefu wa kilometa 10. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo, taratibu za kufanya tathmini ya mali zote zitakazoathiriwa na ujenzi zinaendelea. Mara baada ya kukamilika kwa tathmini, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi wote wanaostahili kwa mujibu wa sheria.