Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Abubakar Damian Asenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilombero
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: - Je, lini Serikali itawalipa fidia wananchi waliopisha ujenzi wa Barabara ya Mchepuko kutoka Ifakara, Kikwawila, Mbasa hadi Lipangalala?
Supplementary Question 1
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na naishukuru Serikali kwa kukubali kwamba inatafuta fedha kwa ajili ya kuijenga barabara hiyo. Wananchi wanasubiri fidia kwa zaidi ya miaka sita katika barabara hiyo na wanaambiwa kwamba tathmini inaendelea. Je, ni lini tathmini hiyo itakamilika?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, katika barabara ya Ifakara Kidatu ambayo Mheshimiwa Rais aliizindua mwaka 2024 mwezi wa Nane, tathmini imeshafanyika, imegundulika kuna wananchi bado wanadai kihalali. Je, wananchi hao nao watalipwa lini?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli hii barabara ya Mchepuo ya Ifakara tathmini ilifanyika muda na ndiyo maana sasa hivi kinachofanyika ni kuihuisha kwa sababu imeonekana hii barabara ilitakiwa ijengwe mapema kwa sababu ya ukuaji wa Mji wa Ifakara, na barabara iliyoko katikati imekuwa haitoshelezi tena mahitaji ya Mji wa Ifakara.
Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la Ifakara – Kidatu wale wote waliokuwa wanastshili kwa mujibu wa sheria walilipwa, lakini kupitia Kamati inayoshughulikia malalamiko chini ya Mkuu wa Wilaya, ilionekana wengine pia waliathirika kutokana na ujenzi ambapo ama barabara ilisogea, ama baada ya kukata magema walionekana wanatakiwa waondoke, kwa hiyo, wanatakiwa walipwe.
Mheshimiwa Spika, tayari tulishapokea taarifa zote za hao watu ambao baada ya kupitia hiyo Kamati ambayo inaongozwa chini ya Mkuu wa Wilaya wanastahili walipwe, na wananchi hao watalipwa hizo fidia zao, ahsante.
Name
Norah Waziri Mzeru
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: - Je, lini Serikali itawalipa fidia wananchi waliopisha ujenzi wa Barabara ya Mchepuko kutoka Ifakara, Kikwawila, Mbasa hadi Lipangalala?
Supplementary Question 2
MHE. NORAH W. MZERU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Je, Serikali ina mpango gani wa kupanua na kuboresha barabara za mikoa zinazopita Morogoro Mjini ili kupunguza ajali za mara kwa mara?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, Mpango wa Serikali kwa sasa, nadhani swali hili nililijibu juzi, kwamba sehemu zote za mji na hasa Mji wa Morogoro upo kwenye mpango wa kujenga barabara zaidi ya nne ili kupunguza msongamano katika mji huo. Kwa hiyo, tayari tumeshaandaa master plan kwa miji yote kuhakikisha kwamba pale ambapo tunahitaji barabara zaidi ya mbili tujenge barabara nne na Mkoa wa Morogoro ni kati ya mikoa hiyo ambayo itanufaika na mpango huo, ahsante.
Name
Twaha Ally Mpembenwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kibiti
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: - Je, lini Serikali itawalipa fidia wananchi waliopisha ujenzi wa Barabara ya Mchepuko kutoka Ifakara, Kikwawila, Mbasa hadi Lipangalala?
Supplementary Question 3
MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Naomba kumwuliza Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba, wapigakura wangu wa Bungu na Nyamisati wanataka kujua, lini barabara ile ya Bungu – Nyamisati itajengwa ukizingatia kwamba upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umeshakamilika?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, naomba tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tulishaanza hatua ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na ninamwomba Mheshimiwa Mbunge baada ya hapa tuonane, kwa sababu kipindi hiki ndiyo tunaandaa mipango kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti inayokuja ili tuweze kuingiza kwenye mipango hii ya 2025/2026, ahsante.
Name
Vita Rashid Kawawa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Namtumbo
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: - Je, lini Serikali itawalipa fidia wananchi waliopisha ujenzi wa Barabara ya Mchepuko kutoka Ifakara, Kikwawila, Mbasa hadi Lipangalala?
Supplementary Question 4
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, je, Serikali imefikia wapi taratibu za ujenzi wa Barabara ya Mtwara Pachani kwenda Lusewa – Magazini mpaka Nalasi – Tunduru? Maana Mwenyekiti mmoja wa kijiji…
SPIKA: Mheshimiwa hiyo ni barabara moja?
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, ndiyo, ni barabara moja, ila inapitia kwenye Kata za Lusewa - Magazini...
SPIKA: Haya, uliza swali lako sasa.
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itajenga Barabara ya Mtwara – Pachani – Nalasi ambayo inapitia katika kata hizo?
Mheshimiwa Spika, juzi nilielezwa na Mwenyekiti wa Kijiji kimoja kwamba mwezi wa Nne niwe nimeanza kuijenga barabara hiyo au watanishughulikia. Je, Serikali inawaeleza nini? (Kicheko)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa...
SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, ngoja kwanza. Mheshimiwa Mbunge maelezo ya sehemu ya pili ya swali lako kidogo yatakuwa nje ya utaratibu wa yale anayoweza kujibu Mheshimiwa Naibu Waziri. Kwa hiyo, ili umweke sehemu nzuri, hebu mwulize swali lako kwa yale anayoweza kuyajibu yeye kama Naibu Waziri wa Ujenzi. Ile sehemu ya pili mwondolee ili asilazimike kukujibu.
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, je, Serikali imefikia wapi kuhusu utaratibu wa kuijenga barabara ya Mtwara - Pachani mpaka Nalasi – Tunduru ambayo inapita kwenye Kata za Mkongo, Ligera, Lusewa, Magazini mpaka Tunduru? (Makofi)
Name
Eng. Ezra John Chiwelesa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Biharamulo Magharibi
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kuna uhitaji mkubwa sana wa kuijenga hii barabara kwa kiwango cha lami. Tulichofanya kama Serikali, kwanza ni kuisanifu barabara yote wakati tunatafuta fedha kuijenga hiyo barabara ambayo ina urefu wa kilomita 300.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, tulichomwahidi Mheshimiwa Mbunge ni kwamba, wakati tunaendelea kutafuta fedha, maeneo yote korofi katika hiyo barabara ambayo huwa yanaleta changamoto tutahakikisha kwamba tunayaimarisha kwa kuyajenga kwa zege ama lami ili wananchi hao wasikwame wakati Serikali inatafuta fedha. Hivyo, mpango huo upo, ndiyo maana tumefanya usanifu kwa barabara yote, ahsante.