Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 152 2025-02-07

Name

Conchesta Leonce Rwamlaza

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question


MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza: -

Je, lini Serikali itatunga sheria itakayolinda utoaji wa huduma za matibabu bure kwa wazee na watoto?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imetunga Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ya Mwaka 2023, ambayo imeanzisha mfuko wa kuhudumia makundi ya watu wasio na uwezo yakiwemo makundi ya wanawake wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.

Mheshimiwa Spika, kuanza kutekelezwa kwa sheria hii kutawezesha makundi yote yakiwemo ya wazee na watoto kupata huduma za matibabu pasipo kuwepo kwa vikwazo vya fedha.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.