Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 155 2025-02-07

Name

Najma Murtaza Giga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA aliuliza: -

Je, Serikali imejipangaje kuhakikisha watoto wachanga wa wasichana wanaoendelea na masomo wananyonya maziwa ya mama kwa wakati?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kulingana na mwongozo wa wanafunzi wanaorejea shuleni baada ya kujifungua, hawaruhusiwi kwenda shuleni na watoto wao na badala yake, mwongozo unawataka wazazi kusaini makubaliano na uongozi wa shule ya kuwajibika kuwalea watoto wa wanafunzi wanaorudi shuleni. Hata hivyo, kupitia elimu nje ya mfumo rasmi, wanafunzi wenye watoto wachanga wanaruhusiwa kunyonyesha kwenye kituo.

Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki katika vituo vya elimu nje ya mfumo rasmi, kwa kujenga chumba maalumu cha watoto katika vituo vyote vipya vinavyojengwa kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari kwa njia mbadala, ambapo katika vituo hivyo, kuna mlezi anayekaa na Watoto, na mwanafunzi mwenye mtoto anapata nafasi ya kunyonyesha mtoto wake kwa wakati, pindi anapohitajika kufanya hivyo. Nakushukuru sana.