Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Najma Murtaza Giga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA aliuliza: - Je, Serikali imejipangaje kuhakikisha watoto wachanga wa wasichana wanaoendelea na masomo wananyonya maziwa ya mama kwa wakati?

Supplementary Question 1

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Naomba kuuliza Serikali, je, haioni umuhimu wa kuwapa muda wa miaka miwili watoto hawa ambao wamejifungua wakiwa shuleni ili wale watoto waweze kupata haki ya msingi ya kiafya kwa kupata maziwa ya mama?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili. Je, Serikali haioni umuhimu wa kurasimisha vituo hivi kwa sababu hili jambo tayari limeshakuwa rasmi katika nchi yetu?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, katika swali lake la kwanza, Mheshimiwa Giga anatoa ushaui kwa Serikali tuweze kuona namna bora ya kufanya iwapo tutatoa nafasi ya miaka miwili. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tumepokea ushauri wake kama Serikali, tutakwenda kuufanyia tathmini ili kuweza kuona ni namna gani tunaweza kutekeleza katika eneo hili.
Mheshimiwa Spika, eneo la pili anazungumzia suala la namna ni gani tunaweza kuruhusu watoto wetu kulelewa kwenye maeneo ya shule. Naomba kumweleza Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu kwamba, Serikali inaendelea kuangalia namna bora ya kufanya kwa kuanzisha au kuimarisha vituo vile vya kulelea watoto kwa maana ya zile daycare centres aidha, ndani ya shule au karibu na shule, ili kuhakikisha kwamba, watoto wetu hawa wanaozaliwa wanaweza kupata malezi bora vilevile na kuweza kuangalia afya zao pindi wanapopata maziwa ya mama. Nakushukuru sana.