Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 157 2025-02-07

Name

Kavejuru Eliadory Felix

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buhigwe

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kumaliza migogoro ya mipaka kati ya wananchi na hifadhi za misitu nchini?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imechukua na inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kutatua migogoro baina ya hifadhi na wananchi nchini. Hatua kubwa ambayo imechukuliwa ni uamuzi wa Mheshimiwa Rais kuunda Kamati ya Mawaziri wa Kisekta toka Wizara nane kubaini na kushauri kuhusu utatuzi wa migogoro hiyo nchini. Kamati hiyo ilibainisha migogoro 975 ambapo migogoro 438 ilibainishwa kuhusu hifadhi za misitu.

Mheshimiwa Spika, katika kutatua migogoro hiyo, tayari Wizara kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania imefanya marejeo ya migogoro hiyo, ambapo migogoro 416, sawa na 95% ya migogoro iliyokuwa imebainishwa imetatuliwa. Migogoro 22 sawa na asilimia tano ipo katika hatua mbalimbali za utatuzi, hususan ile inayohitaji wananchi kuhamishwa kupisha uhifadhi katika maeneo yaliyoonekana yabaki na hadhi ya uhifadhi.