Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 2 Good Governance Wizara ya Viwanda , Biashara na Uwekezaji 24 2025-01-29

Name

Janejelly Ntate James

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANEJELLY J. NTATE aliuliza:-

Je, Serikali imejipangaje kukwamua watumishi walioathiriwa na Mwongozo wa Upandaji Madaraja wa Miaka Minne?

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikichukuwa jitihada mbalimbali za kuoanisha na kuwianisha upandishaji wa vyeo vya watumishi ambapo katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imewapandisha vyeo watumishi 180,000 wakiwemo watumishi walioathirika na zoezi hilo. Aidha, katika utekelezaji wa Ikama na Bajeti ya mwaka 2023/2024, Serikali imewapandisha vyeo watumishi zaidi ya 232,530 wakiwemo walioathirika na zoezi hilo, uhakiki wa vyeti fake na watumishi hewa. Ninashukuru.