Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Janejelly Ntate James
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JANEJELLY J. NTATE aliuliza:- Je, Serikali imejipangaje kukwamua watumishi walioathiriwa na Mwongozo wa Upandaji Madaraja wa Miaka Minne?
Supplementary Question 1
MHE. JANEJELLY J. NTATE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, lakini hawa watumishi waliokumbwa na miaka minne na watumishi wa miaka mitatu sasa wamewapandisha kwa pamoja, wote wamekuwa kwenye position moja. Swali la kwanza; ninaomba Serikali inielezee ni utaratibu gani watachukua kuleta seniority kati ya wale waliokumbwa miaka minne na hawa wa miaka mitatu? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili; walimu waliajiriwa mwaka 2012 walisahaulika, sasa walivyokuja kupandisha vyeo wamepandisha wa mwaka 2013, 2014 na kuendelea. Sasa ni utaratibu gani watachukua ili hawa sasa waonekane kuwa ni ma-senior kwa hawa waliongia miaka iliyofuata? Ahsante. (Makofi)
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Janejelly kwa namna anavyofuatilia mambo ya watumishi.
Mheshimiwa Spika, kuhusu hawa walioathirika na miaka minne, Serikali tumechukua hatua ambako mpaka sasa tumebaki na kiasi kidogo cha watumishi hao ambapo jitihada ambayo inafanyika sasa, katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 tutahakikisha watumishi wote walioathirika na kupanda vyeo miaka minne wanapandishwa kwa mserereko ili waweze kuwa sawa na wengine wale waliowatangulia. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuhusu walimu walioajiriwa mwaka 2012 na watumishi wengine ambao walitakiwa kupanda vyeo mwaka 2016 na promotion zilisitishwa kwa sababu ya uhakiki. Ninaomba nimtoe shaka Mheshimiwa Mbunge, hawa mpaka sasa tuna idadi ya watumishi 6,559 ambayo kwa mwaka huu wa fedha tumepanga bajeti na kama kuna wachache watakaosalia tutawakamilisha katika mwaka wa fedha utakaofuata kwa maana ya 2025/2026. Ninakushukuru sana.
Name
Mwantumu Mzamili Zodo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JANEJELLY J. NTATE aliuliza:- Je, Serikali imejipangaje kukwamua watumishi walioathiriwa na Mwongozo wa Upandaji Madaraja wa Miaka Minne?
Supplementary Question 2
MHE. MWANTUMU M. ZODO: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kuna watumishi wamestaafu toka mwaka 2020 mpaka sasa bado hawajapata mafao yao na kwa kuwa waajiri hawakupeleka fedha kwenye mifuko. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha watumishi hao wanapata mafao yao? Ahsante. (Makofi)
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zodo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni kweli kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya watumishi wanaostaafu wanacheleweshewa kulipwa mafao kwa sababu moja tu baadhi ya waajiri wamekuwa wazembe wa kufikisha taarifa zao katika Ofisi ya Rais, Utumishi ili tuweze kuwa-process kwa wakati na Mheshimiwa Zodo ni moja ya mtu aliyeniletea kero hiyo ofisini na tunaishughulikia.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nitumie Bunge lako kuwataka waajiri wote kwamba wastaafu wanapomaliza muda wao hili jambo sio la dharura, ni jambo ambalo linafahamika, watimize wajibu wao wa kuleta taarifa kwa wakati ili Ofisi ya Rais, Utumishi tuweze kushughulikia suala hilo kwa wakati. Kama kuna wengine watabainika na tulipitisha sheria hapa ndani ya Bunge tutawachukulia hatua kwa sababu kama Serikali hatutaki kuona wastaafu wa nchi hii wananyanyasika wakati wamefanya kazi yao kwa uadilifu kwenda kutumikia Taifa lao. (Makofi)
Name
Issa Ally Mchungahela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lulindi
Primary Question
MHE. JANEJELLY J. NTATE aliuliza:- Je, Serikali imejipangaje kukwamua watumishi walioathiriwa na Mwongozo wa Upandaji Madaraja wa Miaka Minne?
Supplementary Question 3
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Spika, je, Serikali inazungumza nini kuhusu watumishi wanaojitolea katika kada mbalimbali hususani kada ya elimu ambapo kuna watumishi wapo huko wamejitolea kwa zaidi ya miaka sita na kumi sasa hivi? (Makofi)
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana na ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mchungahela, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni kweli kwa mara kadhaa ndani ya Bunge hili mjadala huu umeibuka juu ya vijana wetu wanaojitolea katika sehemu mbalimbali siyo tu kada ya ualimu, lakini tulitoa commitment kama Serikali ndani ya Bunge kwamba tutaenda kufanyia mchakato jambo hili.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nilihakikishie tena Bunge lako, mchakato huu umefika katika hatua ya mwisho na tutaomba ruhusa yako (kibali) pia tukishirikishana na Kamati ili tuweze kuliboresha vizuri na baadaye tutatoa sasa mwongozo katika mwaka huu wa fedha namna ambavyo tuta-accommodate vijana wetu wanaojitolea. Kama Serikali tunatambua kujitolea kwao na tunathamini.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved