Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 2 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 25 2025-01-29

Name

Aloyce John Kamamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buyungu

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka umeme vitongoji visivyokuwa na umeme Wilaya ya Kakonko?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa ridhaa yako, kwa kuwa jana limefanyika tukio la kihistoria la Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Nishati Wakuu wa Afrika, ninaomba kwa ridhaa yako nimpongeze kwa uongozi wake wa mfano uliopelekea Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa maneno ya Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu jana wakati akimkaribisha Mheshimiwa Rais kuzungumza, alisema Tanzania tumepata heshima hii kwa sababu mbili. Moja, kwa umadhubuti wa Mheshimiwa Rais wa kuendeleza sekta ya nishati Tanzania na Afrika; na la pili, kwa Mheshimiwa Rais kutambulika kimataifa kama champion wa nishati safi ya kupikia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa misingi hiyo, ninaomba kumshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa mkutano huu uliowaleta Wakuu wa Nchi na kuweka msimamo wa Mission 300 kuelekea 2030. Heko Afrika! Heko Tanzania! Heko Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Desemba, 2024, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imefanikiwa kupeleka umeme katika vitongoji 146 kati ya 355 sawa na 41.1% vilivyopo katika Wilaya ya Kakonko, Mkoani Kigoma. Aidha, katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, vitongoji 15 vya Wilaya ya Kakonko vinatarajiwa kupelekewa umeme kupitia mradi wa kupeleka umeme kwenye vitongoji. Vitongoji vilivyosalia vitaendelea kupelekewa umeme kupitia miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa.