Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Aloyce John Kamamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buyungu

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka umeme vitongoji visivyokuwa na umeme Wilaya ya Kakonko?

Supplementary Question 1

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA: Mheshimiwa Spika, ahsante kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Aidha, ninaishukuru sana Serikali kwa majibu mazuri.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; wakati utekelezaji huo ukifanyika wa 41%, upelekaji huo haukuzingatia kupeleka umeme kwenye taasisi za Serikali na binafsi hasa misikiti, makanisa na shule za msingi za Serikali. Nini kauli ya Serikali kuhakikisha kwamba taasisi hizo zinapata umeme? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; wakati utekelezaji huu ukifanyika, ulikwenda sambamba na ufyekaji wa mashamba ya miti, migomba, mahindi na kadhalika katika mashamba ya wananchi. Nini kauli ya Serikali kuhakikisha kwamba wananchi ambao mashamba yao yaliharibiwa wanapewa fidia? Ahsante. (Makofi)

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Spika, moja, kuhusu kupeleka umeme kwenye taasisi za Serikali na taasisi binafsi hususan makanisa pamoja na misikiti, Serikali ilikuwa na mradi ambao tulikuwa tunauita UVIKO-19 ambao umepeleka umeme katika taasisi zaidi ya 400. Kwa hiyo, kwa eneo hili la Kakonko, kama bado kuna maeneo ya taasisi ambayo hayajafikiwa na umeme, ninamwelekeza Meneja wa Wilaya kwa bajeti waliyonayo kwa maeneo ambayo yanafikika waendelee kufikisha umeme kwenye taasisi hizo. Sisi kupitia miradi ambayo tunayo ambayo inaendelea na miradi ambayo itaanza kwa mwaka huu wa fedha, tutaangalia maeneo hayo kwa jicho la kipekee.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na fidia kwenye Miradi ya REA, Miradi ya REA ni miradi ambayo imejikita kupeleka huduma kwa jamii na miradi ambayo imetekelezeka kwenye vijiji vyote kwa misingi hiyo, ni miradi ambayo haina fidia. Tunawashukuru wananchi wote kwa utayari wao wa kupisha maeneo ili kupitisha miradi hii ambayo leo imepelekea kufikisha umeme kwenye vijiji 12,318 na tunawaomba waendelee na moyo huo huo kwa Miradi ya REA inayofuatia kwenye vitongoji, ahsante.

Name

Esther Lukago Midimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka umeme vitongoji visivyokuwa na umeme Wilaya ya Kakonko?

Supplementary Question 2

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Je, ni lini Serikali itapeleka umeme katika vitongoji vya Mkoa wa Simiyu ambavyo havina umeme?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante, tunayo miradi ambayo inaendelea ikiwemo miradi ya vitongoji 15, lakini kwa mwaka huu wa fedha tunategemea kuanza mradi mkubwa kupeleka umeme kwenye vitongoji 4,000 na Mkoa wa Simiyu na wenyewe utanufaika. (Makofi)

Name

Minza Simon Mjika

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka umeme vitongoji visivyokuwa na umeme Wilaya ya Kakonko?

Supplementary Question 3

MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itapeleka umeme katika Kitongoji cha Mwanghalaja na Jineli ambavyo havina umeme kabisa?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante, vitongoji ambavyo amevitaja Mheshimiwa Mbunge, nitaenda kuviangalia kama vipo katika miradi inayoendelea na kama havipo basi tutavipa kipaumbele katika miradi inayofuatia ya kupeleka umeme kwenye vitongoji. (Makofi)

Name

Agnes Elias Hokororo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka umeme vitongoji visivyokuwa na umeme Wilaya ya Kakonko?

Supplementary Question 4

MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itapeleka umeme kwenye vijiji vilivyopo katika Wilaya ya Newala, Mtwara Vijijini na Masasi ambavyo mpaka sasa havijaunganishwa? (Makofi)

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, vijiji hivi vya Newala, Mtwara pamoja na Masasi, kote wakandarasi wako site na walikuwa kwenye hatua za mwisho za utekelezaji. Tutaendelea kuhakikisha kwamba tunawasimamia ili kwa muda ambao wamesema ambao ni muda mfupi uliobakia, waweze kukamilisha. Ahsante.

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka umeme vitongoji visivyokuwa na umeme Wilaya ya Kakonko?

Supplementary Question 5

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, kwenye vitongoji 15 ambavyo Mheshimiwa Naibu Waziri, mnapelekea umeme kwa kila jimbo, inasemekana ni vile ambavyo viko karibu na line kubwa, vile ambavyo viko mbali na line kubwa…

SPIKA: Swali, swali, swali.

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, kwa nini hizo fedha zisibaki kwenye hivyo vitongoji hata kama viko nje na line kubwa?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, namna ambavyo miradi hii imekuwa designed, ni kwa ajili ya kupeleka umeme katika maeneo ya vitongoji ambavyo tayari vimepitiwa na line kubwa. Ninampa faraja Mheshimiwa Mbunge, kwa mradi ambao tunaenda kuanza sasa, vile ambavyo viko mbali na line kubwa na vyenyewe vimewekwa kwenye mpango na vitaanza kupatiwa umeme.

Name

Noah Lemburis Saputi Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka umeme vitongoji visivyokuwa na umeme Wilaya ya Kakonko?

Supplementary Question 6

MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itapelekea umeme kwenye vitongoji zaidi ya 58 katika Jimbo la Arumeru Magharibi ambavyo kwa sasa hakuna umeme?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante, tumeanza na vitongoji 15 na katika mradi ambao tutaanza hivi karibuni na vyenyewe tutaongeza idadi ya vitongoji ili wananchi wa eneo la Mheshimiwa Mbunge waendelee kupata umeme.

Name

Shabani Omari Shekilindi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lushoto

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka umeme vitongoji visivyokuwa na umeme Wilaya ya Kakonko?

Supplementary Question 7

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Je, ni lini Vitongoji vya Kwemashai, Muheza, Nkaloi na maeneo mengine yatapata umeme?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kumwambia Mheshimiwa Mbunge kwamba nitaenda kuangalia kama vitongoji hivi tayari tumeshaviweka kwenye mipango yetu na kama havipo basi tutavichukua kwa ajili ya miradi inayofuata ya kupelekea umeme kwenye vitongoji.

Name

Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka umeme vitongoji visivyokuwa na umeme Wilaya ya Kakonko?

Supplementary Question 8

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, Vitongoji vya Wilaya ya Kyerwa zaidi ya 300 havina umeme. Nini mkakati wa Serikali wa kupeleka umeme katika vitongoji hivyo? Ahsante sana.

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, kwa maeneo ambayo yana vitongoji vingi zaidi ambavyo havina umeme, miradi inayofuata vilevile tutakuwa tuna consideration ya maeneo ambayo vitongoji vingi havijafikiwa. Kwa hiyo ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwa Jimbo hili la Kyerwa pia tutaliangalia kwa jicho la kipekee. Ahsante. (Makofi)