Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 2 Finance and Planning Wizara ya Fedha 28 2025-01-29

Name

Janeth Maurice Massaburi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH M. MASSABURI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kutenga bajeti kubwa ya elimu kwa umma kwa masuala mbalimbali yanayotarajiwa kutekelezwa nchini?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa utoaji wa elimu kwa umma kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya jamii. Katika kuhakikisha kuwa jamii inapata uelewa wa kazi mbalimbali zinazotekelezwa na Serikali. Wizara zote na taasisi zake zinasisitizwa kutenga fedha kwenye mafungu yao kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma kuhusu utekelezaji na mafanikio ya shughuli na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa muundo na mgawanyo wa majukumu ya Serikali, jukumu hili linatekelezwa na Idara ya Habari Maelezo, Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa pamoja na vitengo vya mawasiliano Serikalini katika Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi zote. Ahsante sana.