Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Janeth Maurice Massaburi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH M. MASSABURI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutenga bajeti kubwa ya elimu kwa umma kwa masuala mbalimbali yanayotarajiwa kutekelezwa nchini?

Supplementary Question 1

MHE. JANETH M. MASSABURI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina swali moja la nyongeza. Je, Serikali imejipangaje kufanya kampeni kabambe ya elimu kwa umma kwa maeneo ambayo yataleta tija kwa wananchi na hata kwa Taifa? Maeneo kama kilimo cha kisasa, mtu ni afya, usalama barabarani, upandaji wa miti na utunzaji wake, elimu ya makuzi ya vijana na elimu ya mlipakodi. Ninakushukuru. (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, ahsante, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Massaburi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imejipanga katika mikakati mbalimbali kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vyetu vyote,vya habari TV, magazeti na mabango mbalimbali. Ninamwomba Mheshimiwa Mbunge, hata yeye asaidie katika kueleza na kutoa elimu kwa umma kwa mafanikio makubwa sana ambayo yamepatikana hasa Awamu hii ya Sita ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.