Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 2 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 29 2025-01-29

Name

Anton Albert Mwantona

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rungwe

Primary Question

MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:-

Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Barabara ya Katumba Mbambo hadi Tukuyu?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza ujenzi wa Barabara ya Katumba – Mbambo – Tukuyu yenye urefu wa kilometa 83 kwa awamu. Sehemu ya kutoka Lupaso – Mbambo kilometa 20 na kutoka Kabanja hadi Tukuyu kilometa saba ujenzi kwa kiwango cha lami umekamilika. Sehemu iliyobaki ya kutoka Katumba – Lupaso kilometa 35.3 na Mbaka – Kibanja kilometa 20.7 mikataba ya ujenzi imesainiwa na kwa sasa mkandarasi yupo kwenye maandalizi ya kuanza kazi baada ya kulipwa malipo ya awali. Kazi zimepangwa kukamilika mwezi Mei, 2027 kwa sehemu zote mbili. Ahsante.