Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Anton Albert Mwantona

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rungwe

Primary Question

MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Barabara ya Katumba Mbambo hadi Tukuyu?

Supplementary Question 1

MHE. ANTON A. MWANTONA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana kwa majibu mazuri sana ya Serikali kwa sababu kulikuwa na changamoto kubwa sana kwenye hii barabara.
Mheshimiwa Spika, ninaomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, barabara kutoka Kyimo – Ikuti – Ibungu - Ileje lini itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Barabara ya Idweli – Ngumburu – Lugombo ni lini itaanza kujengwa kwa sababu tayari imeshakabidhiwa TANROADS? Ahsante sana.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, Barabara ya Kimo – Ikuti – Luswisi – Katengele – Kalembo hadi Ibungu ni barabara ambayo ipo kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na tulielekezwa iwe imefanyiwa usanifu wa kina.

Mheshimiwa Spika, hivi ninavyoongea barabara hii inaunganisha Mkoa wa Mbeya na Mkoa wa Songwe, Wilaya ya Rungwe na Wilaya ya Ileje. Upande wa Mkoa wa Mbeya, kwa maana ya Kimo hadi Kafwafwa usanifu uko hatua za mwisho na upande wa Ileje, kwa maana ya Kafwafwa – Katengele – Kalembo – Ibungu, usanifu umeshaanza, kwa ajili ya maandalizi kujenga kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, barabara iliyotajwa ambayo sisi tunaitambua kwamba, inaanza pale Nambawano – Ngumburu – Lugombo ni barabara ambayo imepandishwa hadhi kutoka TARURA kwenda TANROADS. Mkandarasi yupo ameshapatikana. Changamoto kubwa ni eneo ambalo mvua kubwa sana inanyesha. Kwa hiyo, anachofanya Mkandarasi sasa hivi ni pale anapopata nafasi kuhakikisha kwamba, hii barabara inapitika, lakini ni kutengeneza barabara yote na kuiweka katika standard ya TANROADS, hasa pale ambapo hali ya hewa itakuwa imekaa sawa. Imeanzwa kutekelezwa mwaka huu wa fedha kwa maana ya TANROADS. Ahsante.

Name

Dr. Josephat Mathias Gwajima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kawe

Primary Question

MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Barabara ya Katumba Mbambo hadi Tukuyu?

Supplementary Question 2

MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniruhusu niulize swali la nyongeza. Ni lini, Serikali itapanua Barabara inayotoka Kiwanda cha Wazo Hill kuteremka kwa Ndevu inayosababisha ajali nyingi kwa sababu, imekuwa nyembamba?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli, swali hili nadhani siyo la kwanza kwa Mheshimiwa Askofu kuuliza. Tulichokifanya ni kuwaelekeza wenzetu wa TANROADS, Mkoa wa Dar es Salaam, ili waweze kuleta taarifa iweze kusanifiwa na kupanuliwa, kwa maana ya kutoka kuwa nyembamba na kuwa pana. Barabara hii ilijengwa muda mrefu na wakati huo watu walikuwa ni wachache, sasa magari yameongezeka hivyo, iweze kukidhi mahitaji ya sasa na kupunguza ajali ambazo zinatokana na wembamba wa barabara ile. Ahsante.

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Barabara ya Katumba Mbambo hadi Tukuyu?

Supplementary Question 3

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Barabara ya kutoka Mogabiri – Nyamongo ni mbovu sana. Mitambo imetoka site na hata service road…

SPIKA: Swali. Swali, swali.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika, nini kauli ya Serikali kupunguza adha kwa watu wangu wa Tarime Vijijini? Ahsante.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, barabara hii ina Mkandarasi yuko site. Ninaomba nitumie nafasi hii kumwelekeza Mkandarasi pamoja na Meneja wa Mkoa wa Mara kuwa, hawatakiwi kutoka site. Aweze kuhakikisha kwamba, anatengeneza zile barabara za diversion, ili barabara iendelee kupitika.

Mheshimiwa Spika, tunachoongea sasa hivi ni tunaandaa fedha kwa ajili ya kumlipa huyo Mkandarasi kwa certificate ambazo amesha-raise kuja kwetu. Ahsante.

Name

Ally Anyigulile Jumbe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyela

Primary Question

MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Barabara ya Katumba Mbambo hadi Tukuyu?

Supplementary Question 4

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE: Mheshimiwa Spika, nini hatima ya ujenzi wa Barabara ya Ibanda – Itungi Port na Iponjola – Kiwira Port? Ahsante sana.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Barabara zote hizo mbili zilipata mkandarasi, lakini alisitishiwa mkataba. Tunavyoongea sasahivi, barabara hiyo iko kwenye hatua za mwisho za manunuzi, kwa maana ya kumsainisha mkandarasi mpya, baada ya taratibu za kutangaza upya na kumpata mkandarasi mpya. Ahsante.

Name

Hamida Mohamedi Abdallah

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Lindi Mjini

Primary Question

MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Barabara ya Katumba Mbambo hadi Tukuyu?

Supplementary Question 5

MHE. HAMIDA M. ABDALLAH: Mheshimiwa Spika, ninaomba kuuliza swali. Ni lini Serikali itakarabati Babaraba inayotoka Ngongo – Ngapa – Rutamba – Milola – Mandawa – Ruangwa kwa sababu, barabara hii imeathiriwa na mvua kubwa ambazo zimenyesha mwaka jana? Ahsante sana?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Barabara zote ambazo ziliathiriwa na mvua mwaka jana zimetafutiwa fedha, ili kuanza kutengenezwa. Nimwelekeze Meneja wa Mkoa wa Lindi kuhakikisha kwamba, maeneo yote ambayo ni kikwazo ahakikishe anampeleka mkandarasi ambaye amepangwa kufanya kazi, ili aweze kutengeneza yale maeneo ambayo ni korofi na magari yaweze kupita. Ahsante.

Name

Samweli Xaday Hhayuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hanang'

Primary Question

MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Barabara ya Katumba Mbambo hadi Tukuyu?

Supplementary Question 6

MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Je, nini mpango wa Serikali wa kuanza ujenzi wa Barabara ya Haydom – Mogitu ambayo usanifu na upembuzi yakinifu umeshakamilika?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, barabara aliyoitaja usanifu umeshafanyika na Serikali inaendelea kutafuta fedha ili iweze kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami. Ahsante.

Name

Capt. (Mst). George Huruma Mkuchika

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Newala Mjini

Primary Question

MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Barabara ya Katumba Mbambo hadi Tukuyu?

Supplementary Question 7

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, Wanaliwale wanataka kusikia Barabara ya Nangurukuru – Liwale ni lini ujenzi wa kiwango cha lami utaanza?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza hii ni kati ya barabara ambazo ziliathirika sana kwenye kipindi cha mvua cha mwaka jana na madaraja mengi sasa hivi wakandarasi wako site. Kwenye maeneo ambayo tulitangaza kujenga tuko kwenye hatua za manunuzi ili kuanza kuijenga kwa kiwango cha lami. Ahsante.

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Primary Question

MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Barabara ya Katumba Mbambo hadi Tukuyu?

Supplementary Question 8

MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Spika, ni lini barabara ya kilometa 10 kutoka Airport kwenda Nyanguge itaanza kujengwa, baada ya mkandarasi kukabidhiwa site toka Mwezi wa Sita mwaka jana, mpaka leo hajaingia?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, barabara aliyoitaja ambayo tunaanza kuijenga kwa kilometa 10 tunachotafuta sasa hivi ni fedha ya kumlipa advance huyo mkandarasi ili aanze kuijenga kwa kiwango cha lami. Ahsante.

Name

Boniphace Nyangindu Butondo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kishapu

Primary Question

MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Barabara ya Katumba Mbambo hadi Tukuyu?

Supplementary Question 9

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Spika, ni lini utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa kutoka Kolandoto kwenda Kishapu, kilometa 20 ambazo zimetengwa katika mwaka huu wa fedha utaanza? Ahsante.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, katika bajeti hii ambayo tunaitekeleza, tulipanga kuanza kuijenga barabara hiyo mwaka huu. Tunachosubiri sasa ni kibali cha kuitangaza, ili iweze kuanza kujengwa. Ahsante.

Name

Daniel Awack Tlemai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karatu

Primary Question

MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Barabara ya Katumba Mbambo hadi Tukuyu?

Supplementary Question 10

MHE. DANIEL A. TLEMAI: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom na Lalago itajengwa kwa kiwango cha lami, pamoja na kuwa mkandarasi amesaini miaka miwili iliyopita? Ahsante.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, barabara aliyoitaja ni moja ya barabara ambazo zimetengenezewa utaratibu maalum ambao utatumika kuzijenga. Ni kati ya zile barabara saba ambazo tulikuwa tunazieleza na sasa imeundwa kamati ya kutafuta utaratibu wa namna ya kuzijenga kwa hatua, ikiwemo barabara hiyo ambayo amesema Mheshimiwa Awack. Ahsante.

Name

Dr. John Danielson Pallangyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Mashariki

Primary Question

MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Barabara ya Katumba Mbambo hadi Tukuyu?

Supplementary Question 11

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Barabara ya Mbuguni, kuanzia Tengeru, hadi Mererani itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami baada ya usanifu na upembuzi yakinifu kumalizika? Ahsante.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, barabara hiyo baada ya kukamilisha usanifu, kipindi hiki cha bajeti, naamini itapangiwa bajeti ili ianze kujengwa kwa kiwango cha lami. Ahsante.

Name

Godwin Emmanuel Kunambi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlimba

Primary Question

MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Barabara ya Katumba Mbambo hadi Tukuyu?

Supplementary Question 12

MHE. GODWIN E. KUNAMBI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza swali dogo la nyongeza kuhusu ujenzi wa Barabara ya Ifakara – Mlimba – Njombe. Ni lini Serikali itawalipa Wakandarasi wote wawili waliopewa kazi ya kujenga kilometa 100 kutoka Ifakara kwenda Chita, ili waanze kazi, yapata mwaka mmoja sasa tangu wasaini mikataba?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, barabara hiyo ina lot mbili na hivi ninavyoongea lot ya kwanza mkandarasi ameshalipwa advance, kwa maana ya malipo ya awali. Kipande cha pili tunatafuta fedha, muda si mrefu tutamlipa, ili kazi ianze kwa lot zote mbili, kwa maana ya vipande vyote viwili, lakini kipande cha kwanza ameshalipwa advance. Ahsante.