Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 13 Water and Irrigation Wizara ya Maji 220 2025-02-13

Name

Dr. Florence George Samizi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Primary Question

MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza: -

Je, lini Serikali itachimba visima virefu vya maji kwenye taasisi za umma hususan mashuleni?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, dhamira ya Serikali ni kuhakikisha huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza inapatikana katika maeneo yote ikijumuisha taasisi za umma zikiwemo shule na vituo vya kutolea huduma za afya. Serikali huzingatia uwepo wa taasisi hizo wakati wa usanifu wa miradi ya maji na hivyo kuhakikisha zinapata huduma hiyo muhimu wakati wa utekelezaji wa miradi. Katika kutimiza azma hiyo, Serikali kupitia miradi mbalimbali iliyotekelezwa imefikisha huduma ya majisafi na salama katika taasisi za umma 31,130 ambapo kati ya hizo, shule za msingi na sekondari ni 25,820 wakati vituo vya kutolea huduma za afya ni 5,310.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kufikisha huduma ya maji kwa taasisi zote za umma nchini kupitia miradi inayoendelea na inayotarajia kujengwa ikiwemo kuchimba visima virefu kadiri itakavyoonekana inafaa.