Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 2 | Union Affairs | Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano | 21 | 2025-04-09 |
Name
Bakar Hamad Bakar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
House of Representatives
Primary Question
MHE. BAKAR HAMAD BAKAR aliuliza:-
Je, kwa kiasi gani Zanzibar inanufaika na fedha zitolewazo na wadau wa maendeleo kupitia Serikali ya Muungano kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada Sura 134 imeweka utaratibu wa namna Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inavyopaswa kunufaika na mikopo, dhamana na misaada kupitia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa muktadha huo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikipeleka fedha zitolewazo na wadau wa maendeleo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuzingatia Sheria hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia fedha hizo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Miradi hiyo imewasaidia wananchi wa pande zote mbili za Muungano kushiriki na kuinua hali zao za kiuchumi pamoja na kuongeza ajira kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Ninakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved