Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 2 Energy and Minerals Wizara ya Nishat 22 2025-04-09

Name

Vincent Paul Mbogo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kusini

Primary Question

MHE. VINCENT P. MBOGO aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka umeme katika Kitongoji cha Lupata Kata ya Kizumbi, Kijiji cha Lyela na Vijiji vya Mwinza na Izinga Kata ya Wampembe?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini imekamilisha kupeleka umeme katika vijiji vyote Tanzania Bara vikiwemo Vijiji vya Mwinza na Izinga vilivyopo katika Kata ya Wampembe. Aidha, Kitongoji cha Lupata kilichopo Kata ya Kizumbi kitapata umeme kupitia mradi wa kupeleka umeme katika vitongoji 15 vya kila Mbunge (Hamlet Electrification Project) na Kitongoji cha Lyela Kata ya Wampembe kitapata umeme kupitia miradi mingine itakayokuja kulingana na upatikanaji wa fedha. Ahsante.