Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Condester Michael Sichalwe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Momba

Primary Question

MHE. VINCENT P. MBOGO aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka umeme katika Kitongoji cha Lupata Kata ya Kizumbi, Kijiji cha Lyela na Vijiji vya Mwinza na Izinga Kata ya Wampembe?

Supplementary Question 1

MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa kunipatia nafasi. Tunashukuru sana Serikali kutusaidia kuwasha umeme kwenye vijiji vyote 72 katika Jimbo la Momba. Pamoja na hilo, ni upi mkakati wa kupeleka umeme kwenye vitongoji vya Tarafa ya Ndalambo, Msangano na Kamsamba?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inao mkakati wa kuendelea kupeleka umeme katika vitongoji na sasa hivi tuna mradi ambao unapeleka umeme katika vitongoji 15 kwa kila Jimbo, ambapo wakandarasi wamemaliza survey na sasa hivi wapo katika hatua ya kupata vifaa ili taratibu nyingine za miradi ziendelee. Katika vitongoji ambavyo Mheshimiwa Mbunge amesema, Serikali inao mkakati wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 9,000 katika mwaka ujao wa fedha. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge, baadhi ya vitongoji katika tarafa hizo tutaziangalia kwa ajili ya kuwapelekea umeme. Ahsante.