Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 2 | Natural Resources and Tourism | Wizara ya Maliasili na Utalii | 29 | 2025-04-09 |
Name
Prof. Patrick Alois Ndakidemi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Vijijini
Primary Question
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI aliuliza:-
Je, Serikali ina mkakati gani wa kupanua wigo wa maeneo mapya ya utalii nchini?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na utalii imekuwa ikitekeleza mikakati mbalimbali inayolenga kupanua wigo wa mazao ya utalii nchini, ili kuvutia watalii wengi zaidi, kuongeza siku za watalii kukaa nchini, kuongeza mapato yatokanayo na shughuli za utalii pamoja na kupunguza utegemezi katika zao la utalii wa wanyamapori nchini. Mikakati inayotekelezwa ni pamoja na kufanya mazoezi ya kubaini vivutio vipya vya utalii nchini; ambapo katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 Wizara imebaini vivutio vipya 337 katika Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi na Kigoma. Aidha, zoezi la kubaini vivutio vipya vya utalii ni endelevu.
Mheshimiwa Naibu Spika, mikakati mingine ni pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi kuendeleza mazao ya utalii ya kimkakati, ikiwemo utalii wa fukwe, meli, mikutano na matukio, malikale na utamaduni na michezo. Mathalani, katika kuendeleza utalii wa meli nchini, Serikali imekuwa ikishirikiana na wadau wa sekta binafsi wenye mtandao mkubwa katika soko la kimataifa la utalii wa meli kutangaza zao hili. Katika kipindi cha Julai, 2024 hadi Machi, 2025 jumla ya meli za kitalii tisa ziliwasili nchini na kuleta watalii 2,944 waliotembelea vivutio mbalimbali vya utalii.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved