Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 3 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 39 2025-04-10

Name

Neema William Mgaya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. NEEMA W. MGAYA aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Njombe – Kibena – Madeke - Lupembe kuelekea Mkoa wa Morogoro?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeanza ujenzi wa Barabara ya Njombe – Kibena – Madeke – Lupembe hadi Mikumi Mkoa wa Morogoro kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Sehemu ya Mikumi hadi Ifakara yenye urefu wa kilometa 109 ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami umekamilika. Sehemu za Ifakara – Mbingu kilometa 62.5 na Mbingu – Chita kilometa 37.5 kazi za ujenzi kwa kiwango cha lami zinaendelea. Kwa sehemu iliyobaki ya Chita hadi Kibena, Mkoa wa Njombe kilometa 246.44, Serikali inaendelea kutafuata fedha kwa ajili ya kuendelea na ujenzi.