Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 3 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 40 2025-04-10

Name

Kavejuru Eliadory Felix

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buhigwe

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga viwanda vya kuchakata zao la migomba?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Zao la Migomba ama ndizi ni miongoni mwa mazao makubwa katika Wilaya ya Buhigwe na maeneo mengine nchini. Kutokana na tafiti zilizofanywa duniani zao la migomba linaweza kutumika kutengeneza bidhaa kama vile vikapu, mikeka, kofia, chakula cha mifugo, mbolea, nguo, karatasi, nyuzi, dawa za asili na malighafi za kujengea lakini pia matunda yake hutumika kama chakula.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) na Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) ina teknolojia ya kuchakata migomba kwa ajili ya chakula cha mifugo na viwanda vya kutengeneza mvinyo, unga wa lishe, keki na crispy zinazotokana na ndizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua umuhimu wa uongezaji thamani zao la migomba pamoja na ndizi, Serikali kupitia SIDO imepanga kuanzisha kongani ya zao la migomba na ndizi katika halmashauri, ikiwemo Halmashauri ya Buhigwe ili kuongeza mnyororo wa thamani kwa zao hilo. Aidha, zao hili ni miongoni mwa mazao yatakayoongeza thamani nchini kupitia mpango maalum wa kuendeleza viwanda wa miaka mitano unaotarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia mwaka wa fedha 2025/2026 hadi 2029/20230. Nakushukuru.