Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 21 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 269 2025-05-09

Name

Deodatus Philip Mwanyika

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Njombe Mjini

Primary Question

MHE. NEEMA W. MGAYA K.n.y. MHE. DEODATUS P. MWANYIKA Aliuliza: -

Je, lini mpango wa ujenzi wa Chuo cha Utalii katika Mji wa Njombe utaanza?

Name

Dr. Pindi Hazara Chana

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer


NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII Alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali katika mpango wake wa kuimarisha utoaji huduma katika sekta ya utalii na ukarimu nchini, imeendelea kuimarisha Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kwa kununua nyenzo za kisasa zaidi za ufundishaji pamoja na kufungua kampasi za chuo hicho katika maeneo mbalimbali nchini ili kusogeza huduma za chuo hicho karibu na wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini Serikali imeanza kuchukua hatua mbalimbali za kufungua kampasi mpya ambapo Wizara imepata eneo la takribani ekari 27 katika Kijiji cha Ikisa, Kata ya Uwemba, Halmashauri ya Mji Njombe. Aidha, hati ya umiliki wa eneo hilo tayari imepatikana na Wizara inatarajia kuanza ujenzi wa kampasi hiyo hivi karibuni kadiri fedha zitakavyopatikana. (Makofi)