Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Neema William Mgaya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA W. MGAYA K.n.y. MHE. DEODATUS P. MWANYIKA Aliuliza: - Je, lini mpango wa ujenzi wa Chuo cha Utalii katika Mji wa Njombe utaanza?

Supplementary Question 1

MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwa kuwa Wizara ndiyo mpo kwenye mchakato wa kutegemea kupata fedha ili muanze kujenga; na kwa kuwa kuna taasisi nyingi sana ambazo zinalitaka hilo eneo ili kuweza kuliendeleza. Je, mpo tayari kuliachia hilo eneo tukafikiria kuwapa hizi taasisi nyingine kwa kuwa ninyi bado hampo tayari?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA, NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Serikali inaendesha shughuli zake kwa mipangilio na hivyo kama nilivyoeleza kwenye jibu la msingi, wakati wowote tunaenda kuanza ujenzi na hatuwezi kuliachia hilo eneo kwa ajili ya taasisi nyingine kwa sababu tayari tulishaliingiza kwenye mpango wa kuliendeleza.

Name

Kiswaga Boniventura Destery

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Magu

Primary Question

MHE. NEEMA W. MGAYA K.n.y. MHE. DEODATUS P. MWANYIKA Aliuliza: - Je, lini mpango wa ujenzi wa Chuo cha Utalii katika Mji wa Njombe utaanza?

Supplementary Question 2

MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwanza tunaishukuru Serikali kwa kuanza kujenga Chuo cha Utalii katika Mkoa wa Iringa, lakini sasa ninaona kimesimama. Je, ni lini ujenzi huo utaendelea?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA, NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa mwenyekiti, Chuo cha Utalii tawi la Iringa tayari kimeshaanza kujengwa na kwa sasa kupitia bajeti hii itakayoanza hivi karibuni chuo kile kinaenda kuendelezwa ujenzi wake ili kikamilike haraka kwa ajili ya wananchi. (Makofi)

Name

Kavejuru Eliadory Felix

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buhigwe

Primary Question

MHE. NEEMA W. MGAYA K.n.y. MHE. DEODATUS P. MWANYIKA Aliuliza: - Je, lini mpango wa ujenzi wa Chuo cha Utalii katika Mji wa Njombe utaanza?

Supplementary Question 3

MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana; Mkoa wa Kigoma umejaaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii tukiwa na mbuga ambazo zina wanyama wa pekee chimpanzee, Gombe na Mahale na vivutio vingine. Je, Serikali iko tayari kujenga kampasi ya chuo cha utalii katika Mkoa wa Kigoma? (Makofi)

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba kwa sasa tunajaribu kuendelea kufanya tafiti ya maeneo ambayo tunaweza tukawekeza vyuo vya utalii. Ninapokea ombi la Mheshimiwa Mbunge na kwamba Wizara itaenda kufanya tafiti na ikijiridhisha itaanzisha ujenzi wa chuo ambacho Mheshimiwa Mbunge ameomba kijengwe.