Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 13 Energy and Minerals Wizara ya Nishat 158 2025-04-28

Name

Shabani Omari Shekilindi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lushoto

Primary Question

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza:-

Je, lini Vitongoji vya Hendelo, Ngaloi na Muheza, Lushoto, vitapata umeme?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Kitongoji cha Muheza kilichopo Kijiji cha Rwandai, Kata ya Rwandai, kitapatiwa umeme kupitia Mradi wa Kupeleka Umeme Vitongojini, Awamu ya Pili B, ambao zabuni ya kuwapata Wakandarasi imetangazwa na inatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni. Vitongoji vingine vilivyosalia, ikiwemo Hendelo na Ngaloi vitaendelea kupelekewa umeme kupitia miradi ijayo kulingana na upatikanaji wa fedha. Ahsante.