Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Shabani Omari Shekilindi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lushoto

Primary Question

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza:- Je, lini Vitongoji vya Hendelo, Ngaloi na Muheza, Lushoto, vitapata umeme?

Supplementary Question 1

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika, Vitongoji vilivyopimwa toka mwaka juzi, ambavyo ni Vitongoji vya Kwemishai, Kwemkashi, Kwebarabara, Magunga, Zeta, Kiuzai, Ula, Mpalai pamoja na Mzizima, ukizingatia vitongoji hivi vina Taasisi za Dini na Shule za Msingi. Swali la kwanza; je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi yake hiyo ya kuweka umeme katika vitongoji hivyo nilivyovitaja kwa kuwa, vina sifa zote za kupata umeme?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kila Mbunge aliahidiwa vitongoji 15; hivyo vitongoji 15 tulishawahamasisha wananchi na tukawaambia wanapata umeme. Je, ni lini utekelezaji wake utaanza? Ninakushukuru.

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ninaomba nijibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge, kwa pamoja, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika vitongoji ambavyo amevitaja, hivyo vyote vimewekwa katika mradi wa kupeleka umeme kwa vile vitongoji 15 vya kila Mbunge. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kama ambavyo tumeahidi, basi ndio hivyohivyo vitongoji vitapatiwa umeme.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na mkandarasi, nilitaja hapo awali, ipo mikoa mitatu ambayo wakandarasi walikuwa hawajapatikana. Mbeya, Singida pamoja na Tanga, Lushoto, kwa Mheshimiwa Mbunge, Mkandarasi ameshapatikana ataenda kutambulishwa wiki hii na atakabidhiwa site. Ahsante.