Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 19 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 250 2025-05-07

Name

Dr. Florence George Samizi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Primary Question

MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza:-

Je, lini Serikali itakarabati Skimu za Umwagiliaji za Nyendara, Muhambwe, Kumbanga, Mgondogondo na Kigina, Muhambwe?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini, ikiwemo Skimu za Nyendara, Muhambwe, Kumbanga, Mgondogondo na Kigina zilizopo Jimbo la Muhambwe.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, imeanza kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, kwa ajili ya ukarabati wa Skimu za Nyendara, Muhambwe, Kumbanga, Mgondogondo na Kigina zilizopo Jimbo la Muhambwe. Utekelezaji wa kazi za upembuzi yakinifu umefikia 70% na unatarajia kukamilika ifikapo Juni, 2025. Baada ya usanifu kukamilika skimu hizo zitatangazwa mara moja, kwa ajili ya ukarabati. Ahsante sana.