Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 18 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 235 2025-05-06

Name

Ally Juma Makoa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kondoa Mjini

Primary Question

MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka gari la zimamoto Wilaya ya Kondoa ili kukabiliana na majanga ya moto yanayotokea mara kwa mara?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kuboresha utendaji kazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika kulipatia vitendea kazi kupitia mradi wa ununuzi wa magari na vifaa vya kuzima moto na uokoaji wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 100 kutoka Kampuni ya ADEX iliyopo Dubai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huo utawezesha kupatikana kwa vitendea kazi mbalimbali ikiwemo magari 150 ya kuzima moto na uokoaji yatakayotoa huduma katika Wilaya zote nchini ikiwemo Wilaya ya Kondoa, ahsante. (Makofi)