Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 18 Water and Irrigation Wizara ya Maji 236 2025-05-06

Name

Jafari Chege Wambura

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rorya

Primary Question

MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza:-

Je, lini Mradi wa Maji Miji 28 Rorya - Tarime utakamilika?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Miji 28 wa Rorya - Tarime uliopo Mkoani Mara. Kazi zinazotekelezwa katika mradi huo ni pamoja na ujenzi wa dakio (intake) katika Ziwa Victoria lenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 29 kwa siku, ujenzi wa miundombinu yenye uwezo wa kutibu maji lita milioni 28 kwa siku, ulazaji wa bomba umbali wa Kilometa 90, ujenzi wa matenki yenye jumla ya ujazo wa lita milioni 10 sanjari na ujenzi wa kituo kimoja cha kusukuma Maji (booster station).

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa 12.5%, na kwa mujibu wa mkataba unatakiwa kukamilika mwezi Julai, 2025 na kunufaisha wananchi 460,885 waishio katika Wilaya za Rorya na Tarime, ahsante.