Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 19 Water and Irrigation Wizara ya Maji 251 2025-05-07

Name

Abeid Ighondo Ramadhani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Kaskazini

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:-

Je, lini Serikali itasambaza maji salama katika Kitongoji cha Gairu, Kijiji cha Sagara ambacho wanatumia maji yenye chumvi?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, lengo la Serikali ni kuhakikisha huduma ya majisafi na salama inapatikana kwa wananchi waishio vijijini, ikiwemo Kitongoji cha Gairu, ambacho kwa sasa kwa sehemu kinapata huduma kupitia Skimu ya Maji ya Sagara. Aidha, serikali imechimba visima na kujenga point sources katika Jimbo la Singida Kaskazini, kwenye Vijiji vya Mrama, Mwakinchenche, Ikiwu na Mukulu, kama mpango wa muda mfupi wa kuhakikisha huduma ya maji inapatikana. Pia, Serikali inaendelea na uchimbaji wa visima vingine katika Vijiji vya Mangida, Minyenye, Misinko na Kitongoji cha Gairu, ambapo utekelezaji wake unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2025.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea vilevile na Tathimini ya Upanuzi wa Skimu ya Maji ya Sagara kupeleka maji Kitongoji cha Gairu. Mradi utatekelezwa kwa Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026, ahsante.