Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2015-2020 | Session 15 | Sitting 37 | Energy and Minerals | Wizara ya Nishati | 312 | 2019-05-28 |
Name
Desderius John Mipata
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nkasi Kusini
Primary Question
MHE. DESDERIUS J. MIPATA aliuliza:-
Vijiji vya Sintali, Nkana, Nkomachindo na Katani viko kwenye mpango wa kupata umeme wa REA Awamu ya III lakini mpaka sasa hakuna kazi zinazoendelea:-
Je, ni lini kazi hiyo itaanza?
Name
Subira Khamis Mgalu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishati, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Desderius John Mipata Mbunge wa Nkasi Kusini kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, jumla ya vijiji 51 vitapatiwa umeme katika Wilaya ya Nkasi ikiwa ni pamoja na vijiji 12 vya Jimbo la Nkasi Kusini vya Ntuchi, Tambaruka, Chima, Chatelekesha, Isasa, Kingombe, Ntemba, Nkomolo II, Kasapa, Kisula, Namansi na Kasu B. hadi kufikia mwezi Mei, 2019 umeme tayari umeshawasha katika vijiji vya Chala, Chima, Chala Isasa na Ntemba. Jumla ya wateja wa awali 77 wameunganishiwa umeme. Aidha, mkandarasi anaendelea na kazi katika vijiji 9 viliovyosalia.
Mheshimiwa Naibu Spika, kazi za mradi katika Jimbo la Nkasi Kusini vinahusisha ujenzi wa kilometa 29.65 za njia ya umeme wa msongo kilovoti 33; kilometa 28 za njia ya umeme wa msongo wa kilovoti 0.4; ufungaji wa transfoma 14 na uunganishwaji wa wateja wa awali 324. Gharama za kazi hiyo inakadiriwa kufikia shilingi bilioni 2.15.
Mheshimiwa Naibu Spika, vijiji vya Sintali, Nkana, Katani na Nkomachind vitapatiwa umeme kupitia mradi wa REA III mzunguko wa pili unatarijiwa kuanza mwezi Julai, 2019 na kukamilika mwezi Juni, 2021.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved