Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 11 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi | 140 | 2023-04-20 |
Name
Mussa Ramadhani Sima
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Mjini
Primary Question
MHE. FRANCIS I. MTINGA K.n.y. MHE. MUSSA R. SIMA aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya mchepuko kutoka Kisaki – Unyamikumbi - Unyambwa hadi Mtipa?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mussa Ramadhan Sima, Mbunge wa Singida Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali tayari imekamilisha Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa kina wa barabara ya mchepuko katika Mji wa Singida (Singida Bypass) kutoka Kisaki – Unyamikumbi – Unyambwa hadi Mtipa yenye urefu wa kilometa 46. Kwa sasa Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved